KUDHIBITI MCHWA SHAMBANI NA MAJUMBANI...
Tumia Viwatilifu Vifuatavyo.
1)Nuvan( Inatengenezwa na Ultravetis East Africa.
2) Confidol WG 70 au SL ( Bayer Crop science). .
Pamoja na Viwatilifu vinginevyo vilivyoelekezwa Matumizi ya Mchwa.
Kumbuka:
🔹Mchwa wanaishi kwa Utawala Mkali. Hivyo ukitumia Viwatilifu vyenye Harufu kali utawauwa walio Nje Tuuu.kisha wa Ndani watahama na Kutoboa Upande Mwingine.
🔹 Confidol Haina Harufu. Ila ikimpata Mchwa anaanza Kuwashwa na anapatwa na Mhaho😄😄😄 hivyo atakimbia hovyo hovyo na Kuwapakaa wenzake. Ndivyo itakavyoenea Sumu.
Fanya yafuatayo:
⏩Chimba sehem ya Kichuguu kisha mwagia Maji ya kawaida Mpaka Palowane.
⏩Chukua Mchanganyiko wako wa Confidol/ Nuvan kisha mwagia sehemu hiyo kwa wingi. ..
⏩Kama ni kwenye Kitalu ,Changanya Confidol(Imidacloprid) na Maji kulingana na Kipimo kisha Mwagilia Kitalu na Cane. Amini hutoona Mchwa kwa Miaka 10.
⏩Wadudu wengine kwenye Kitalu watakufa .
Wasiliana Nami kwa Mahitaji yako ya Jumla na Rejareja.
Felicasto Agrocare for Reliable and Sustainable Services