DONDOO ZA MATUMIZI SAHIHI YA 'SOLO' ZA KUPIGIA VIWATILIFU SHAMBANI.
🤏Kabla ya Msimu kuanza ni vema kuhakikisha uko na vitendea Kazi Muhimu,Mojawapo ni Bomba lakupulizia Viwatilifu ( Knapsack sprayer.
🤏 Wakati unajiandaa kwenda Kupuliza Viwatilifu,Fanya yafuatayo.
🔹Kagua kifaa Chako
🔹Kaza Nozo kwa usahihi na funga Nozo kulingana na aina ya kiwatilifu unachoenda Kupuliza . Zipo Nozo kwa Ajili ya Magugu ( Nozo ya Mkato) , Zipo kwa ajili ya Wadudu na viuwakuvu ( Round Nozo) ,Zipo kwa ajili ya Kupuliza kwenye Mimea mirefu kama mbaazi /Miti ( Nozo ya Njano)
🔹Fanya ukaguzi wa Mwendo ( Calibration)
🔹Kisha Jaza Maji nusu ya Solo lako.
🔹Unapaswa uwe na kindoo kidogo cha shambani,kisha Weka Maji kama Lita 3 hivi kwenye kindoo.
🔹Chukua Kiwatilifu Chako na pima kiwango cha Dawa kisha Weka ndani ya kindoo na chukua Mti kisha koroga mpaka Mchanganyiko wako uchanganyike vema.
🔹Kisha mimina ndani ya Solo,na Tikisa kwa Muda wa Dakika 1 kisha Jazia Maji kwa kiwango kilichobakia na utikise tena...
⚠️Usitumie Mdomo wako kuzibulia Nozo iliyoziba
⚠️Usijaze Maji Kwenye solo kupita kwenye shingo yake ( Pale Palipoandikwa 15ltr,16ltr,au 18ltr au 20ltr) ukizidisha unajiweka katika hatari ya kumwagikiwa na Kiwatilifu.
⚠️ Hakikisha Maji ni Masafi wakati wa kuchanganya.
⚠️Baada ya kumaliza Kupuliza,safisha Solo lako kwa Maji safi kisha liinamishe livuje Maji kisha nenda lakihifadhi stoo.
⚠️Linda Panya asije kulitoboa.
Felicasto Agrocare for Reliable and Sustainable Services