FAHAM MAGONJWA YA HOHO KWA UFUPI SANA.
1)Batobato- Husababishwa na Virusi ambapo Huenezwa na Wadudu wanaofyonza kama Inzi weupe .
Dalili zake: Kudumaa Mmea na Majani Kujikunja.
Udhibiti: Panda Mbegu zinazostahimili Ugonjwa Huu kama Yolo Wonder.
Fanya Crop rotation.
2)Chule( Anthracnose)- Ugonjwa wa Ukungu unaosababishwa na Fangasi.
Dalili: Madoa Madoa kwenye Tunda na Jani.
Udhibiti: Tumia Mbegu zenye uwezo wa kukinzana na Ugonjwa.
Puliza viuwakuvu vyenye Uwezo wa Kutibu.
3)Bakadoa( Bacterial Leaf Spot)
- Husababishwa na Vimelea vya Magonjwa,na Husambazwa kupitia Mbegu,Mvua na Umande.
Dalili: Majani kuwa na Madoa Madoa yenye Rangi ya Njano.
- Kingo za Jani kuwa na weupe na Taratiiibu Kahawia.
Udhibiti: Panda Mbegu zinazostahimili Ugonjwa Huu.
Puliza viuwakuvu vyenye Uwezo wa Kutibu.
4) Bakajani ( Phytophthora Blight)
- Huenezwa kwa njia ya umwagiliaji Mbovu wa Maji Shambani.
Huathiri sehem zooote za Mmea.
Dalili: Majani Kuchomeka na kuwa na Mabaka ya Kahawia.
- Hoho kuoza.
- Miche michanga Kuoza
Udhibiti: Panda Mbegu zinazostahimili Ugonjwa Huu.
Puliza viuwakuvu vyenye Uwezo wa Kutibu.
5) Mnyauko Fusaria (Fusarium wilt)
Huu ni Ugonjwa unaosababishwa na Fangasi, kwa Mimea michanga
Dalili: Mimea Michanga Kunyauka , Majani ya Mimea Kunyauka na kufa kabisaaa.
Udhibiti: Tumia Mbegu safi,na Puliza viuwakuvu vyenye Uwezo wa Kutibu.
6) Mnyauko wa Bacteria - Ugonjwa unaosababishwa na Vimelea vya Bakteria.
Dalili: Mmea wote Kunyauka ghafla pasipo Majani kubadilika Rangi,
Udhibiti: Hakikisha unatupa Mbali Masalia ya Hoho .
7) Ubwiri Unga (Powdery Mildew)
-Husababishwa na Vimelea vya Fangasi. Na hupendelea maeneo yenye Joto .
Dalili: Unga Unga Rangi ya Kijivu kwenye Majani Juu na Chini.
Udhibiti: Tumia Viuwakuvu vyenye Uwezo wa Kutibu kama Hexaconazole.
8) Blossom End Rot.( kuoza kitako)
Husababishwa na upungufu wa viini lishe( Calcium) Pamoja na Umwagiliaji Mbovu
Udhibiti: Weka Mbolea zenye Calcium Pamoja na Umwagiliaji mzuri.
9)Kata Kiuno (Damping off)
Hupelekea Mimea hasa Miche Kuoza chini na kukatika.
Udhibiti: Hakikisha Maji Hayatuami shambani. Tumia viuwakuvu vyenye Uwezo wa Kutibu.
Felicasto Agrocare for Reliable and Sustainable Services