HERBICIDES

 Active ingredient: 2,4-D Dimethylamine Salt 720SL

M.O.A : Contact & Systemic Herbicide.

KAZI YAKE.

👎Ni Kiuagugu penyezi chenye uwezo wa Kuangamiza Magugu aina ya Majani Mapana ( Mboga Mboga) na Kuacha Mazao yakiwa salama.

👎2,4-D inauwezo wa Kuua Majani Mapana ndani ya masaa 12 tuu tangu uipulize. Pindi uipulizapo hutoa Majibu muda huo huo kwa Majani kuanza kuonyesha kuinama.

👎 Hupulizwa kwa Mls 150-250 / 20ltr za Maji.

👎Unaweza kuichanganya na Sumu za Kuuwa Pungapunga na Ndago.

👎Tumia Nozzle ya Kupigia Sumu za Magugu . Nozzle Mkato

👎Hutumika kwenye Palizi ya Mpunga na Mahindi , Miwa( kwa tahadhali )

👎Unaruhusiwa kuingia shambani na kuendelea na shughul zingine baada ya masaa 48 tangu upulize.

👎Unaweza kufanya Mavuno siku 30 baada ya Kupuliza.( Pre - Harvest Interval)

Usichanganye na Mbolea za Aina yoyote. Na usubiri siku 7 baada ya Kupuliza ndo unaweza kuweka Mbolea.

Tunazo Aina kadhaa za 2,4-D kama Vile; Aminoforce 2,4-D, Sura 2,4-D, Rafiki 2,4-D n.k..




Karibuni sana Felicasto AgroCare Co Ltd kwa Huduma Bora zenye kukidhi Mahitaji yenu...


Previous Post Next Post

Contact Form