Dalili zinazojionyesha Kwenye Mmea Kulingana na Aina ya Upungufu wa Virutubisho.
Nitrogen
Dalili:
🔸Mimea Shamban hukua kwa taabu sana.
🔸Majani yanakuwa na kijani mpauko.
🔸Sukumawiki na kabichi majani yanakuwa na mchanganyiko wa rangi ya njano.
🔸Majani ya chini ndiyo huathiriwa kwanza.
🔸 kiwango cha maua kuchanua hupungua au kuchelewa.
Suluhisho.
🔸Ongeza kiasi cha kutosha cha mbolea za asili.
🔸Panda mimea inayosaidia kuongeza nitrojen kama lablab, desmodium(figiri) na lusina.
🔸Weka mboji, samadi na mbolea ya Chenga au ya maji yenye nitrojen kwa wingi.
Phosphorous
Dalili:
🔸Mahindi, maharage na mbogamboga haikui vizuri.
🔸Majani hugeuka na kuwa rangi ya kijani, bluu na zambarau.
🔸Matunda hubakia kuwa madogo.
🔸Inaweza kuharibu mizizi au kukosekana kwa Nitrojeni.
Suluhisho
🔸 Tumia mbolea asili ya maji yenye phosphorus.Au weka Mbolea ya Chenga yenye Phosphorus Nyingi.
Potassium
Dalili:
🔸Majani yanakuwa na rangi ya njano kama yanakauka kuzunguka. 🔸Kuchanua kwa shida na kutokuwa mpango mzuri wa matunda.
🔸Mmea unashambuliwa na magonjwa kirahisi.
Suluhisho.
🔸Boresha udongo wako kwa kutumia mimea yenye virutubisho vya potassium.
🔸 weka majivu kwenye shamba lako.
🔸Weka Mbolea yenye Virutubisho husika kwa Wingi.
Calcium
Dalili
🔸Shina la Mmea kuwa dhaifu sana .
🔸Matunda Machanga na Mauwa kupukutika.
🔸kuoza kwa Matunda kwenye Kitako.
Suluhisho
🔸Weka Mbolea zenye uwiano Mzuri wa Calcium..
🔸Samadi Pia inaweza kuwa Msaada.
Magnesium
Dalili
🔸Majani ya Juu ( Developing tissue) kuwa ya Njano.
Suluhisho
🔸Weka Mbolea yenye Virutubisho vya Magnesium.
Boron
Dalili
🔸Jani la Mmea hubadilika Kuwa Jeupe Kabisaaa.
Suluhisho
🔸Tumia Mbolea yenye Boron kwa w
ingi.
Kama Unachangamoto yoyote Karibu Felicasto Agrocare tutakushauri na Kukupatia Huduma Bora Kabisa.