Tujikumbushe Upuliziaji wa Viuwadudu kwa ajili ya Inzi mweupe/ Vipepeo ( White Flies)
Chagua kiwadudu Mathubuti kwa ajili ya Kumwangamiza Mdudu huyu. Sio k
ila Kiwatilifu kinaweza Kumwangamiza kama ilivyozoeleka awali,.
▶️Jaza Maji nusu ya Bomba lako( Knapsack Sprayer)
▶️Weka Maji kama Lita Moja au mbili kwenye kindoo Cha Shambani Cha Kuchanganyia Viwatilifu.
▶️Pima kiwango cha Kiwatilifu Chako kisha Weka kwenye kindoo na ukoroge na Kijiti mpaka ichanganyike vizuri,
▶️Mimina ndani ya Bomba na Utikise vizuri.
▶️Jazia Maji kiasi kilichobaki kisha Tikisa tena.
▶️Piga Mstari mmoja kuzunguka Shamba lote Pande zote kwa ajili ya kuweka wigo/ Uzio wa Wadudu wasiruke Nje ya Shamba.
▶️Baada ya kuweka Uzio sasa Anza Kupuliza Kiwatilifu Chako.
⚠️ Hakikisha unapuliza Asbuhi sana kabla Wadudu hawajatawanyika Au Jioni sana baada ya wadudu kurudi kwa aJili ya Maandalizi ya Kulala ...
Ahsante.👏
Felicasto Agrocare for Reliable and Sustainable Services.